Wednesday, September 19, 2012

MKESHA WA KUSIFU NA KUABUDU

Wapendwa ndugu zangu nachukua fursa hii kuwasalimu kwa siku ya leo ambayo tumepata Neema ya kukuta. Kuna siku niliwaahidi kuwa nitawaletea picha za usiku wa mkesha. Sasa wakati na siku imefika ya kuwaonesha kwa sehemu kupitia picha za mnato. na tukipata nafasi utaweza  kuiona tena kwa kupitia njia ya video.

Mtumishi wa Mungu Dada Marther akitibua wingu la sifa. Haaaaa, ilikuwa ni balaa kwelikweli,tulimwona El Shadai kwa kiwango cha juu sana. Hata kama ulikuwa hutaki kusamama na kumsifu Mungu ungejikuta ukiamka mwenyewe bila kupenda.
Na hapo Mtumishi wa Mungu Dada Assia alikuwa akumtumikia Mungu kwa namna ambaya Mungu alimuwezesha kuyafanya. Kwa kweli Tulimwona Mungu kwa Namna ya ajabu.
  
Watumishi wa Mungu wapigaji vyombo walifanya mambo ya ajabu sana na kumdhihirisha Mungu kupitia kipawa walichopewa na Mungu wao. Kwa kweli drums zilitulia,guitor la base lilikuwa linaleta utamu hasa, bila kuvisahau vinanda viwili vilivyo leta ladha nzuri tofautitofauti

Friday, September 14, 2012

Tuesday, September 11, 2012

WAPENDWA WOTE MLIOSHIRIKI KATIKA MKESHA

WA KUSIFU NA KUABUDU.

 

Tunapenda kuwashukuru watu wote mlio ungana nasi katika mkesha wa kusifu na kuabudu uliofanyika katika kanisa la Lutheran usharika wa Ruanda,Jimbo la Mbeya iliyopo Dayosisi ya Konde. Kwa kweli tuliona Utukufu  wa Bwana ukishuka kwa namna ya ajabu sana. Mungu  awabariki.

Skukrani zetu ziwaendee watu woye waliofanikisha shughuli nzima ya maandalizi.

Kamati ya Maandalizi kwa ujumla chini ya Mwenyekiti wake Ndg TUNTUFYE ARNOLD.

Ndugu wanavyuo wote waliojitoa kwa ajili ya maandalizi yote.

Ndugu wote waliotoka nje ya mkoa kwa ajili ya maandalizi na kuhudhuria.

Pia kwa watu wote walio jitokeza kuungana nasi kwa pamoja ili Tulitukuze Jina la Bwana,MUNGU AWABARIKI. 

Mungu akitupa uzima siku si nyingi mtaziona picha zilizopigwa wakati wa kusifu na kuabudu,mtuwie radhi ni kutoka na sababu zilizopo juu ya uwezo wetu tumeshindwa kuwaletea picha hizo.