Tuesday, November 13, 2012

"SI LAZIMA WAENDE ,WAPENI NINYI CHAKULA" MATHAYO 14:13-21

UTANGULIZI
   " SI LAZIMA WAENDE, WAPENI NINYI CHAKULA" Ni maneno ya Bwana Yesu alipokuwa akiwaambia wanafunzi wake wakati alipokuwa na makutano makubwa ya watu waliomfuata katika faragha na faragha hiyo ilifanyika nyikani, mahali ambapo hapakuwa na chakula, na hali wakiwa katika mfungo wa siku ya tatu. Hiyo siku ya tatu walikuwa na njaa na ndipo wananafunzi wakamwambia Yesu kuwa watu wana njaa unaonaje waende wakanunue vyakula, ndipo Yesu akawaambia wapeni ninyi chakula, ndipo wakajibu hatuna ila tuna SAMAKI WAWILI  NA MIKATE MITANO TU.
   Kwa mtumishi wa Mungu ni lazima kuwa na chakula cha akiba mda wote. Akiba ya chakula ni kwa ajili ya kundi la Bwana. Kwani ukiwa mtumishi katika eneo lolote lile ulilopewa na Mungu jua kuwa watu wa eneo hilo wako chini yako. Kutegemea kwao kunategemea sana na wewe umekaaje na sheria ya Bwana. MALAKI 2:7 "Kwa maana yapasa midomo ya kuhaniihifadhi maarifa, tena yawapasa watu kuitafuta sheria kinywani mwake (mtumishi wa Mungu) kwa kuwa yeye ni mjumbe wa Bwana waMajeshi"
     Hivyo kama Mtumishi wa Mungu ni wajibu wako kutafuta chakula kwa ajili ya eneo lako na si chakula tu bali pia kiwepo chakula cha akiba . Mtu akija kwako akiomba chakula inakubidi uumpe haijalishi unacho au hauna your responsible to give him/her. Kwanini? kwa sababu eneo unalopewa na Mungu anakupa chakula cha kutosha kwa kipindi fulani, na kama amekupa hiyo kwa kipindi hicho unatakiwa pia kuwa na akiba ya dharura. Ndha unafahamu nini maana ya dharura. Dharura jambo linalo tokea lisiloterajiwa katika sehemu hiyo bila kuwa na wakati maalum,sehemu maalum taarifa maalum. Kwa mfano ukipokea mshahara ukapanga bajeti yako, na ukanunua kila kitu ndani, halafu unakuta hujabakiwa na kitu ndani, ghafla unashangaa kumetokea msiba kijijini uliko zaliwa halafu kijiji hicho na takribani kilometa 700, halafu wewe ni wa muhimu sana katika msiba huo na ukiangalia mfukoni huna fedha, hatimaye unaishia kukopa. Ndivyo hata ulimwengu wa Roho kulivyo. Mungu akikupa chakula kwa ajili ya watu wa eneo lako, anakupa  kwanza akili ya kuweza kukitumia chakula hicho, kwani chakula ni cha wakati na wakati. Leo hii ukimpa chakula kisicho cha wakati mtu atakiona kuwa hakimfai  kwa nini? ukisoma MHUBIRI 3:1 " Kwa kila jambo kuna majira yake, na wakati kwa kila kusudi chini ya mbingu" Kwa hiyo inatakiwa kuwa na chakula cha wakati na cha akiba pia.
ITAENDELEA..........

Friday, November 9, 2012

MABADILIKO YA BLOG HII KIMWONEKANO

HABARI NDUGU ZANGU.
      NAFIKIRI MTAKUWA MMEONA MABADILIKO YALIYO TOKEA KATIKA BLOG YETU. KAMA UNA MAONI YOYOTE BASI TUANDIKIE KUPITIA UKURASA WETU WA FACEBOOK   . lusajo media production. NA KAMA UMEIPENDA BASI BOFYA KATIKA KITUFE CHA "LIKE". 
      NI KUTOKANA NA MAENDELEO YA KI-TEKNOLOJIA. SASA UNAWEZA KUPATA HABARI HIZI KUPITIA LUGHA MBALIMBALI DUNIANI. 

      KILICHO BAKI NI KUTUOMBEA!!!!!!