COMPUTER IMETOKEA WAPI?
Mpenzi Msomaji wa Blog hii nakukaribisha sana katika Makala yetu ya Kwanza kabisa inayoelezea maisha ya Computer tokea kipindi inavumbuliwa mpaka leo tunaitumia. Hii ni historia ya Computer iliyopo katika kumbu kumbu mbali mbali za kimtandao na vitabuni. Hivyo nakukaribisha sana usome na uelewe ili tunako elekea kusiwe kugumu sana
Kompyuta ilijulikana kwa mara ya kwanza mnamo karne ya 19
kupitia Profesa jina lake aliitwa Prof CHARLES BABBAGE alikuwa ni Mwangereza na alikuwa mtaalamu wa
Hesabu, Mwanafalsafa, Mhandi wa Mitambo ( Mechanical Engineer) na ndiye
aliyeleta wazo la kompyuta.
Unapozungumzia kompyuta unazungumzia hatua tatu au Vizazi
vikuu vitatu. Na kila hatua ina Miaka yake na Maendeleo ya Kiteknolojia.
Prof. Charles Babbage
KIZAZI CHA KWANZA
(1937-1946)
Mnamo mwaka 1937 Computer ya kwanza
ilitengenezwa na Dr John V. Atanasoff na
Bw Clifford Berry. Na Computer hii iliitwa ATANASOFF-BERRY COMPUTER (ABC).
Fig 1. ATANASOFF-BERRY COMPUTER (ABC).
Mnamo mwaka 1943, Computer iitwayo
COLOSSUS ilijengwa na wanajeshi
Fig 2. COLOSSUS COMPUTER
Maendeleo madogo madogo
yaliendelea na ikiwa lengo hasa ni kutengeneza Computer kubwa iliyoitwa
ELECTRONIC NUMERICAL INTERGRETOR AND COMPUTER (ENIAC).
Fig 3. ELECTRONIC NUMERICAL INTERGRETOR AND COMPUTER (ENIAC).
*Computer hii ilikuwa na uzito wa Tani 30
*Ilikuwa na vacuum Tubes 18,000 ambazo zilikuwa
zinafanya kazi
* Kwa mara ya kwanza hii computer ilianza
kwa kutoa mwanga hafifu sana
*Na computer hii iliweza kufanya kazi moja tu
na haikuwa na Operating System (Windows 7, Windows XP n.k)
KIZAZI CHA PILI
CHA COMPUTER (1947-1962)
Katika kipindi hiki au kizazi hiki cha pili cha computer,
Computer zilikuwa zikitumia zaidi TRANSISTOR badala ya VACUUM TUBES kwa sababu
ziliaminika zaidi.
Mnamo mwaka 1951, Computer ya kwanza kwa ajili ya biashara,
iligunduliwana kutangaza kwa jamii. Na computer hi iliitwa UNIVERSAL AUTOMATIC MAC HINE (UNIVAC 1).
Fig 4. UNIVERSAL AUTOMATIC MAC HINE (UNIVAC 1).
Mnamo mwaka1953, Shirika
lakimataifa linaloshughulikia Mashine za kibiashara, International
Business Machine (IBM) lilitengeneza computer ambazo ziliitwa IBM 650 na 700.
Fig 5. IBM 650 computer
Fig 6. IBM 700 computer
Katika kipindi hiki lugha za kitaalamu za kikompyuta (Programming
Language)zilikuwazimekwisha tengenezwa zaidi ya 100
*Computer hizi zilikuwa na
kitunza kumbu kumbu(Memory Drive)
*Computer
hizi zilikuwa na Operating System (Windows
kwa lugha inayo fahamika sana)
*Na
katika kipindi hiki zilikuja teknolojia za Printer na Tape kwa ajili ya
kuhifadhi kumbu kumbu hifadhiwa. (Hard
Copies)
KIZAZI CHA TATU
CHA COMPUTER (1953-LEO).
Kutokana na maendeleo makubwa na ubunifu wa hali ya juu
sana,Computer iliendelea kupunguzwa ukubwa wa kimwonekano, kutoka ukubwa wa jengo mpaka computer ya kubebwa
kiganjani. Computer za sasa Zina uwezo mkubwa sana ukilinganisha na computer za
kipindi kile, zinaweza kufanya kazi nyingi kwa wakati mmoja.
Mnamo mwaka 1980, Microsoft ilizaliwa na kuleta operating
system iliyokuwa ikiitwa Microsoft Disk Operating System (Ms DOS)
Mnamo mwaka 1981, IBM alitangaza computer za kutumia
maofisini na majumbani ambayo iliitwa Personal Computer (PC)
Mnamo mwaka 1984, Apple alileta Computer iliyoitwa Macintosh
PC
Na mwaka 1990 Microsoft ilizindua Operating System iliyoitwa
WINDOWS ambayo asilimia kubwa ndiyo inayotumika sana maofisini, majumbani, nah ii operating system huongezwa ubora kila
baada ya kipindi Fulani. Hii ni kutikana na kuzidi kugundulika zaidi kwa
teknolojia mpya.
Mpenzi Msomaji wangu anatumaini nitakuwa nimekupa mwanga japo
kwa ukaribu, ili uweze kupata picha ya wapi computer ilitokea. Kwa maswali
zaidi, maoni , ushauri tupigie namba hizo juu.
Imeandaliwa na
Lusajo Mwaihabi
mwaihabilusajo@yahoo.com
No comments:
Post a Comment